Monday, July 17

Waumini wawili wafa maji wakibatizwa

Rombo. Waumini wawili wa Kanisa Siloam  wamekufa maji wakibatizwa katika Mto Ungwasi wilayani Rombo baada ya mmoja wao kupandisha mapepo na kuwatumbukiza majini.
Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Agnes Hokororo amethibitisha tukio hilo lililotokea leo, Julai 16 saa sita mchana. Ubatizo huo ulifanyika  kwenye kina kirefu cha mto huo.
Amesema wakati ibada ya ubatizo mmoja wa waumini aliyepandisha mapepo alimtumbukiza mmoja wa watu waliokuwa wakisubiri kubatizwa na mchungaji.
Hokororo amesema muumini mmoja alipoona mwenzake ametumbukizwa majini aliamua kumwokoa, ndipo aliyepandisha pepo alipowashikilia wote wawili ndani ya  maji na kuwasababishia kifo.
Amesema watu watatu akiwamo mchungaji wa kanisa hilo lililopo katika Kijiji cha Mandechini wanashikiliwa.

No comments:

Post a Comment