Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Ushiriki watanzania katika uwekezaji wa katika sekta ya madini na kilimo ni mdogo kutokana na mifumo iliyopo na kufanya nchi kwa wazawa kushindwa kunufaika.
Akizungumza katika mdahalo ulioandaliwa na Taasisi Isiyo ya Kiserikali inayojighulisha na Utafiti wa Kisera kwa ajili ya Kukuza Sayansi , Teknolojia na Ubunifu (Stipro), Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushiriki Watanzania katika sekta ya Uwekezaji wa Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi Kiuchumu (TNBC) , Esther Mmbaga amesema kuwa baraza limeunda kitu cha kuweza kufatilia mikataba na sera namna ya wazawa wanavyoshiriki katika uwekezaji.
Amesema ushiriki watanzania katika uwekezaji kuanzia ajira na hata bidhaa zinazozalishwa nchini hazitumiki kwa wawekezaji kutokana na madai kuwa hazina ubora.
Mmbaga amesema kutokana na ukosekanaji wa ushiriki Baraza litaweka utaratibu kwa kila kinachofanyika nchini chi ya uwekezaji watanzania waweze kushiriki au kufanya ubia kwa teknolojia kuandaa utaalam wa uzalishaji wa taaluma.
Amesema kuwa tafiti hizo ndizo zinafanya baraza kufanyia kazi katika kuangalia wazawa wanavyonufaika na uwekezaji unaofanywa nchini.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali inayojighulisha na Utafiti wa Kisera kwa ajili ya Kukuza Sayansi , Teknolojia na Ubunifu (Stipro) Bitrina Diyamett amesekuwa utafiti huo ulijikita kuangalia uwekezaji kwa kiasi gani watanzania wanashiriki.
Amesema watu wanafanya uwekezaji nchini lakini hawanunui bidhaa za ndani na kuonekana watanzania sio sehemu ya uwekezaji hali ambayo inahitaji kuangalia sera pamoja na mikataba.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ushiriki Watanzania katika sekta ya Uwekezaji wa Baraza la Taifa uwezeshaji wananchi Kiuchumu (TNBC) , Esther Mmbaga akizungumza katika ufunguzi wa mdahalo uliojikita kuangalia uwekezaji kwa kiasi gani watanzania wanashiriki atika masuala ya uwekezaji kwenye mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Costech jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali inayojighulisha na Utafiti wa Kisera kwa ajili ya Kukuza Sayansi , Teknolojia na Ubunifu (Stipro) Bitrina Diyamett akizungumza juu utafiti wao waliofanya kupitia taasisi hiyo katika kuangalia watanzania kunufaika katika masuala ya uwekezaji .
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mzumbe , Profesa Honest Ngowi akizungumza juu masuala ya uwekezaji na utafiti uliofanywa na Taasisi ya Stipro jana jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau katika wa mdahalo uliojikita kuangalia uwekezaji kwa kiasi gani watanzania wanashiriki uliofanyika katika ukumbi wa Costech jana jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment