Mpango huo utakaozinduliwa Julai 31, unaratibiwa na shirika la kimataifa la WaterAid ambalo linajihusisha na miradi ya maji na usafi wa mazingira.
Mkurugenzi wa mipango wa shirika hilo, Abel Dugange, amesema katika kipindi cha miaka mitano nguvu kubwa itaweka katika kuhakikisha wananchi wanapata maji safi, salama na yenye uhakika.
Amesema hapo awali suala la uhakika wa upatikanaji wa huduma za maji lilikuwa halipewi kipaumbele lakini katika mkakati huo mpya watalitilia mkazo suala hilo.
"Tanzania bado tuna safari ndefu, takwimu zinaonyesha kuwa hadi sasa ni asilimia 50 pekee ya watu ndiyo wanapata maji ndiyo sababu katika mkakati huu tunaongeza nguvu kuhakikisha wengi wanafikiwa na huduma hiyo," amesema.
Kuhusu suala la vyoo, amesema takwimu zinaonyesha kuwa hadi sasa mtu mmoja kati ya watatu hatumii choo bora.
"Ipo haja ya kutolewa kwa elimu kuwawezesha wanajamii wenyewe kubadilika. Tabia ya kunawa mikono, kutumia vyoo bora inzie ndani ya mtu tangu akiwa mdogo, "amesema.
Kwa upande wake Kaimu Mkugenzi wa kitengo cha habari Wizara ya Maji, Athuman Sharif, amesena serikali itandelea kushirikiana na wadau kuhakikisha inafikia malengo iliyojiwekea katika kuwafikishia maji watanzania.
No comments:
Post a Comment