Saturday, July 29

Kasoro zaanza kugundulika kwa madiwani waliohama Chadema





Sakata la madiwani watatu waliojiuzulu wa chama Cha Demokransia na Maendeleo (Chadema) katika jimbo la Hai, limechukua sura mpya baada ya kubainika kuwepo kwa tofauti ya majina na kata za madiwani gao waliojiuzulu
Akizungumza na waaandishi wa habari, mwenyekiti wa halmashauri ya hiyo, Helga Mchomvu, alikiri kupokea barua za madiwani watatu kujiuzulu nyadhifa zao na kuhama chama.
Hata hivyo, amesema baada ya kuzipitia barua hizo kwa undani alibani kasoro kadhaa ikiwamo ya majina majina ya kata kurtoshabihiana na majina ya madiwani husika.
Akifafania, Mchimvu alisema barua iliyondikwa  Julai 25 mwaka huu na aliyekuwa diwani wa kata ya mnadani, Ernest Kimath, inaonyesha kuwa alikuwa diwani wa kata ya Weruweru na si kata ya Mnadani.
“Pia barua ya tarehe hiyo hiyo iliyoandikwa na aliyekuwa  diwani wa kata ya Weruweru, Abdallah Chiwili, ina maelezo yanayoeleza kuwa alikuwa diwani wa kata ya Mnadani si Weruweru huku mwisho wa barua hiyo ukiwa na jina na sahihi ya Chiwili ”alisema Mchomvu na kuongeza:
“Kinachoonekana  ni kuwa barua zile ziliandaliwa na mtu mmoja na wahusika waliweka sahihi bila kujali maelezo yaliyomo ndani yake.”
Mchomvu alisema barua ya aliyekuwa diwani wa kata ya Machame Magharibi Goodluck Kimaro niliyoandikwa mnamo Julai 25 mwaka huu haina upungufu wowote.
“Pamoja na upungufu hup lakini mimi kama mwenyekiti wa halmashauri inayotokana na Chadema nimeridhiria maamuzi yao na sasa tunasubiri maelekezo mengine juu ya hatima ya kata hizo,” alisema.
Akizungumzia hatua ya madiwani hao kujiuzulu kaimu mwenyekiti wa ChademaA wilaya hiyo, Joe Nkya, alisema kitendo hicho ni usaliti kwa chama na kinaonyesha wanacheza na rasilimali za watanzania.
“Kiongozi wa kuchaguliwa anapojiuzulu lazima uchaguzi ufanyike upya na rasilimali za watanzania zinatumika. Uchaguzi katika kata moja unaweza kugharimu zaidi ya shilingi milioni 30 ambapo zingesaidia katika shughuli za maendeleo,” alifafanua.
Nae mjumbe wa kamati tendaji ya wilaya ya Chama hicho, Simoni Mnyampanda alisema kuwa hawana wasiwasi na kuondoka kwa madiwani hao kwa sababu walikuwa kama namba tu katika utendaji wao.

No comments:

Post a Comment