Akizungumza kabla ya uzinduzi huo leo Julai 19, Mama Samia amesema Serikali imetekeleza mapendekezo 25 kati ya 92 yaliyotolewa kwenye ripoti hiyo na kusisitiza kwamba itatekeleza mapendekezo yote.
Amewataka wadau mbalimbali kuendelea kufadhili utekelezaji wa ripoti hiyo ambayo inalenga nyanja mbalimbali za uchumi na utawala bora.
"Serikali imeshatoa maelekezo kwa watendaji kuandaa ripoti za kila mwaka juu ya utekelezaji wa mapendekezo yaliyobainishwa kwenye ripoti. Tutaendelea kusimamia utekelezaji wake mpaka mwisho," amesema Mama Samia.
Makamu wa Rais amesema ripoti hiyo ina mchango mkubwa katika kufikia azma ya serikali ya kuwa nchi ya viwanda kwa sababu imebainisha pia mbinu za kuinua uchumi.
Ametaja baadhi ya mambo yaliyofanyiwa kazi kuwa ni kutatua migogoro ya ardhi, kuongeza uzalishaji na usambazaji wa umeme, kuboresha mfumo wa elimu, kusimamia suala la jinsia na kupiga vita rushwa.
No comments:
Post a Comment