Wednesday, July 19

Profesa wa CCM ndiye meya Dodoma



Dodoma. Madiwani wa Manispaa ya Dodoma leo wamemchagua Diwani wa Kuteuliwa (CCM), Profesa Devis Mwamfupe kuwa meya wa manispaa hiyo baada ya kumgaragaza Diwani wa Kikombo (Chadema), Yona Kusaja kwa kura 50.
Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi amemtangaza Mwamfupe kuwa meya baada ya kupata kura 50 huku Kusaja akiambulia kura nane kati ya kura 58 zilizopigwa katika uchaguzi huo ulioshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mdema na kamati yake ya ulinzi na usalama.
Uchaguzi huo umefanyika baada ya Jaffary Mwanyemba kuondolewa katika uongozi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za mradi wa maji katika kata ya Zuzu na matumizi mabaya ya madaraka.







No comments:

Post a Comment