Nairobi. Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema kwamba uchaguzi utafanyika mwezi ujao kama ulivyopangwa licha ya wapinzani kuweka vikwazo.
Akizungumza katika eneo la Ukunda, Kwale, Rais Kenyatta amesema ni lazima uchaguzi ufanyike Agosti 8 kama ulivyopangwa.
“Nimegundua upinzani hauko tayari kwa uchaguzi tangu mwaka jana walipoanza kushambulia Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC),” amesema.
Rais Kenyatta akiwa ameandamana na naibu wake William Ruto amesema.’Hatutaruhusu kuahirishwa kwa uchaguzi’.
“Tunatangaza kwamba Wakenya watachagua viongozi wawapendao Agosti 8 ili waendelee na shughuli zao za kila siku,” amesema.
Viongozi hao wa Jubilee wamedai Muungano wa National Super Alliance (Nasa) hauko tayari kwa uchaguzi bali unahitaji kunyakua mamlaka kupitia 'mlango wa nyuma’.
Upinzani wamedai mbele ya Mahakama Kuu kwamba, tume ya IEBC imeshindwa kuzingatia sheria inayoitaka kutangaza mbinu mbadala zitakazotumiwa endapo mitambo ya kielektroniki itakwama.
No comments:
Post a Comment