Harare, Zimbabwe. Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe amemzawadia shemeji yake, Junior Gambochuma zawadi ya Dola 60,000 (Sh 133.2milioni) katika sherehe ya siku yake ya kuzaliwa.
Pia watoto wake (Gambochuma) wamempa dola 10,000 kama zawadi. Gazeti la Serikali la nchi hiyo, The Herald limeeleza.
Katika sherehe iliyofanyika shambani kwa Rais huyo mwenye umri wa miaka 93, Mugabe amesema anampa zawadi hiyo shemeji yake kwa kuwa amekuwa mlezi wa kiroho wa watoto wake.
Gambochuma, ni dada mkubwa wa mke wa Mugabe, Grace.
Mugabe alisema Gambochuma ambaye ni mchungaji ni mtu muhimu katika familia hiyo kwa kuwa amekuwa akiwalea watoto wake kwa kuwafundisha dini.
No comments:
Post a Comment