Taarifa iliyotumwa na kitengo cha mawasiliano cha ACT-Wazalendo, leo imeeleza kuwa ziara hiyo itaanza Julai 17 na mkoa wa kwanza utakuwa ni Mara.
“Katika ziara hiyo, Maganja atafuatana na katibu wa kamati ya kampeni ya uchaguzi Mohamed Massaga, pia watakutana na kamati ya uongozi ya mkoa na majimbo yote ya mkoa” imesema
Mikoa mingine itakayofikiwa katika ziara hiyo ni Simiyu (Julai 19), Shinyanga (Julai 20),Mwanza(Julai 21),Manyara (Julai 23),Arusha(Julai 24) na Kilimanjaro (Julai 25)
“Baada ya ziara hiyo na itakayofuatiwa na tathmini ya kina Mwenyekiti Maganja atamalizia mikoa iliyosalia ya Tanzania bara kabla ya kuelekea mikoani kwa ajili ya kujitambulisha rasmi,” imesema
Taarifa hiyo imesema ziara hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa kiongozi huyo ambaye alipokea kijiti cha uongozi kutoka kwa Mama Anna Mghwira, aliyeondolewa katika nafasi hiyo na kamati ya uongozi ya chama baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli kuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment