Kiungo Mkabaji, Papy Kabamba Tshishimbi anayekipiga Mbambane Swallows ya Swaziland, anatarajia kumalizana na Yanga SC wakati wowote kuanzia sasa baada ya kufaulu vipimo vya afya.
Mchezaji huyo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwenye umri wa miaka 27, amefanyiwa vipimo hivyo katika zahanati ndogo ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya daktari, Nassor Matuzya.
Mchezaji huyo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwenye umri wa miaka 27, amefanyiwa vipimo hivyo katika zahanati ndogo ya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya daktari, Nassor Matuzya.
“Yanga ni timu kubwa, hatuwezi kusubiri hadi mkataba wake uishe, tunamsajili mara moja,” alisema Nyika
Miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa katika kikosi hicho cha Mzambia, George Lwandamina ni Golikipa wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Ramadhani Kabwili, kipa Mcameroon, Youthe Rostand aliyesajiliwa kutoka African Lyon, beki Abdallah Hajji ‘Ninja’ kutoka Taifa Jang’ombe, kiungo Pius Buswita kutoka Mbao FC, na mshambuliaji Ibrahim Ajib kutoka kwa mahasimu, Simba SC.
No comments:
Post a Comment