Saturday, July 29

Kalonzo asema amani baada ya uchaguzi ina masharti



Mgombea mwenza wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance (Nasa), Kalonzo Musyoka, amesema hatima ya amani ya baada ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 8, 2017 ina masharti.
"Haina mashiko kutuambia tudumishe amani bila kufafanua ni amani ya aina gani. Msimamo thabiti ni kuwa amani hupaliliwa na mazingara mwafaka ya kuonyesha watu kuwa kuna msingi wa kushinikiza kudumisha amani,” alisema Kalonzo wakati wa mahojiano na kituo kimoja cha habari juzi.
Kalonzo ameitwisha mzigo Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) akisema kuwa ili kuwepo na amani baada ya uchaguzi ni lazima uchaguzi huo uandaliwe kwa njia ya haki, huru na ya wazi.
“Siyo tusikie kuna masuala ya wizi wa kura, kuna mikakati ya ubaguzi katika usimamizi wa kura na masuala mangine mengi maovu ambayo hayazingatii uadilifu wa kura na kisha unamwambia mwathiriwa aweke amani,” alisisitiza Kalonzo.
Kalonzo aliweka wazi kwamba Nasa itakubali matokeo yatakayotangazwa kwa masharti kuwa uchaguzi umeandaliwa katika njia ya haki na inayozingatia kuwapa Wakenya uhalali wa sauti yao na kura yao.

No comments:

Post a Comment