Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam kuhusu ushirikiano wa Benki hiyo na TICTS ambapo wateja wa kampuni hiyo wataweza kufanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini ambapo katika kufanikisha jambo hilo benki imefungua Tawi lake katika jengo la PSPF linalopakana na geti la ofisi za TICTS, huku muda wa huduma ukiongezwa kuanzia saa 8:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku kwa siku za kazi, na saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kwa siku ya Jumamosi. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe na kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe wakisaini mkataba wa makubaliano wa kushirikiana katika kuhakikisha wateja wa TICTS wanafanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini. Mkataba huo ulisainiwa jana katika tawi la Ecobank lililopo PSPF Towers jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe (katikati) wakipeana mkono baada ya kutia saini ya mkataba wa makubaliano wa kushirikiana katika kuhakikisha wateja wa TICTS wanafanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini. Mkataba huo ulisainiwa jana katika tawi la Ecobank lililopo PSPF Towers jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia (kulia) ni Mkurugenzi wa Usimamizi wa fedha wa Ecobank Africa, Isaac Kamuta, Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai (wa pili kushoto), na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Kampuni ya TICTS, Donald Talawa (kushoto).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Raphael Benedict (kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa TICTS Jared H. Zerbe (katikati) wakibadilisha mikataba ya makubaliano ya kushirikiana katika kuhakikisha wateja wa TICTS wanafanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank hapa nchini. Mikataba hiyo ilisainiwa jana katika tawi la Ecobank lililopo PSPF Towers jijini Dar es salaam. Anayeshuhudia kushoto ni Katibu Mkuu wa Tanzania Freight Forwarders Association (TAFFA), Tony Swai.
Benki ya Ecobank Tanzania leo imeingia katika ushirikiano rasmi na TICTS, ambapo wateja wa kampuni hiyo wataweza kufanya malipo yao kwa haraka na ufanisi zaidi kupitia tawi lolote la Ecobank.
Benki hii imeanzisha mfumo ambao utawawezesha wateja wa TICTS kufanya malipo yao papo kwa hapo kupititia mfumo huu rahisi. Huduma hiyo itakuwa inapatikana kwa wateja wa Ecobank na wasio wateja wa benki hii.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaaam leo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ecobank, Raphael Benedict alisema benki hiyo inataka kuhakikisha huduma ya uagizaji na utoaji mizigo bandarini katika Bandari ya Dar es Salaam inakuwa rahisi zaidi na ya haraka zaidi kwa wateja wa TICTS.
Benedict aliongeza kuwa ili kuwezesha jambo hilo, Ecobank Tawi la PSPF ambalo linapatikana karibu na geti la ofisi za TICTS, limeogeza muda wa huduma zake na sasa litakuwa likifunguliwa saa 8:00 asubuhi hadi saa 4:00 usiku kwa siku za kazi, na saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni kwa siku ya Jumamosi.
Hata hivyo mipango ya benki hiyo ni kupanua zaidi huduma zake hadi siku ya Jumapili. Kwa maana hiyo, muda ulioongezwa utawawezesha wateja kuwa na wigo mpana zaidi wa kufanya shughuli zao na kukamilisha shughuli za upakuaji wa makontena.
Alisema kupitia mfumo mpya wa benki wa kidijitali, Eckobank Tanzania imekuwa katika mchakato wa kukamilisha hatua za utoaji huduma kwa saa 24 za malipo kwa wateja wa TICTS.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania International Container Services (TICTS), Jared Zerbe alisema kampuni hiyo imekuwa ikijitahidi katika kuboresha huduma zake ili kuendana na mahitaji ya wateja wake.
“Tunafuraha sana kuingia ushirikiana huu na Ecobank ambao utatusaidia kuboresha huduma zetu za kila siku. Kwa kuboresha huduma zetu, tumefungua akaunti yetu Ecobank ambapo wateja wataweza kufanya malipo yote ya huduma za TICTS. Pia Benki imefungua tawi jipya jirani na ofisi zetu za TICTS ghorofa za jengo la PSPF pembezoni mwa Barabara ya Sokoine Drive ili kurahisisha utoaji huduma kwa wateja,” alisema.
“Wateja wetu wanashauriwa kutumia matawi matano ya Ecobank yaliyopo jijini Dar es Salaam kwa huduma za malipo ya huduma mbalimbali za TICTS.”
TICTS na Ecobank watatambulisha njia mpya ya malipo kupitia mtandao wa simu ya mkononi na vituo vya mauzo kwa pamoja kwa mtindo mwingine wa malipo kupitia Ecobank. Taarifa itatolewa mara mpango huo utakapokamilika. Pia wateja watajulishwa kuhusu sehemu na tarehe ya kuhudhuria semina kwa wateja ili kukuza uelewa kuhusu malipo kwa mtandao na kupunguza usumbufu jinsi ya kutumia huduma za kibenki kwa mtandao.
No comments:
Post a Comment