Sunday, June 18

Mabodi aitaka CCM iendelee kufanya sera za ushindani wa maendeleo


Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amesema CCM itaendelea kufanya ushindani wa sera za maendeleo zitakazowanufaisha wananchi wa makundi yote mijini na vijijini.
Kauli hiyo ameitoa leo (Jumamosi) wakati akifungua mafunzo ya Wanawake na Uongozi kwa wanachama na viongozi wa Umoja wa Wanawake (UWT), Mkoa wa Mjini huko Amani Zanzibar.
 Dk Mabodi amesema wananchi wa Zanzibar kwa sasa wanachohitaji ni siasa za ushindani wa kisera katika kukuza kipato cha mwananchi mmoja mmoja hadi taifa kwa ujumla.
Amesema taifa lolote linalotamani kuendelea kiuchumi ni lazima wananchi wake wakubali kwa vitendo dhana ya siasa za ustaarabu katika kudumisha amani na utulivu wa nchi ili kufanya kazi za kujiongezea kipato na kukuza uchumi wa nchi.

No comments:

Post a Comment