Moshi. Mkazi wa Mailisita wilayani Hai, Paulo (35) amekufa maji baada ya kuzama katika mto Kikafu, dakika chache baada ya kubadili dini na kubatizwa na maji ya mto huo kwa imani ya dini ya Kikristo.
Paulo ambaye jina lake la awali lilikuwa Issa Juma kabla hajabadili dini, alifariki Jumapili iliyopita katika mto huo, wakati shamrashamra za kubatizwa kwake zikiendelea pembeni ya mto.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi lililazimika kuwakamata wachungaji wawili wa kanisa la Efatha waliombatiza lakini waliachiliwa baada ya Polisi kujiridhisha kuwa Paulo alikufa maji baada ya kubatizwa.
Habari zilizothibitishwa na Polisi, zimeeleza baada ya kubatizwa saa 8:30 mchana na wakati waumini wakiimba kwa ajili ya kurudi kanisani, ndipo Paulo na mwenzake waliamua kurudi kuogelea.
No comments:
Post a Comment