Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Freeman Mbowe amesema uchovu ndiyo sababu iliyomfanya kuugua ghafla jana na kulazwa katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili, jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika maandamano ya kumsindikiza mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa, kuchukua fomu jana, Mbowe aliugua ghafla eneo la Manyanya, Kinondoni na kulazimika kukimbizwa Muhimbili ambako amelazwa hadi leo.
Hata hivyo, mwanasiasa huyo ambaye anawania ubunge katika jimbo la Hai kupitia Chadema amewahakikisha wanachama na wafuasi wa Ukawa kuwa afya yake ni njema na huenda akaruhusiwa kutoka hospitalini ndani ya saa 48.
Akizungumza na Mwananchi jana, Ofisa Uhusiano wa Muhimbili Aminieli Aligaesha pamoja na kukiri kulazwa kwa mwanasiasa huyo, hakutaka kuweka hadharani kilichokuwa kinamsumbua Mbowe.
No comments:
Post a Comment