Askari wanne na Wananchi Kadhaa Wameuawa. Hadi kufikia saa
hii (3:00 pm) kuna taarifa kwamba ofisiza CCM (maeneo ya Mdenganamadi na
Majengo) zimechomwa moto; askari wanne wameuawa pamoja na wananchi kadhaa.
Wananchi wanatumia baruti za kulipulia samaki kuwalipua majengo na
askari.Hatari iliyopo ni kuchomwa kwa jengo la ofisi za mkuu wa mkoa. Yote haya
ni kupinga bomba la gesi kujengwa kuelekea DSM.
Habari zilizofika muda huu zinaripoti kwamba hali sio nzuri
huko Mtwara, kwa ufupi hali ni tete na hakuna amani, mabomu ya machozi
yanarindima muda huu na huduma zote za kijamii zimefunngwa hakuna usafiri,
masoko, maduka na bar zote zimefungwa, daladala, Taxi na Bodaboda hazifanyi
kazi. Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na
wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali
nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.
Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa
ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam ilihali Waziri wa Nishati
akisoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe na kusema bomba la gesi
linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam Wananchi wa Mtwara wacharuka!
Daraja la Mikindani limevunjwa hakuna mawasiliano Mtwara na
Dar es salaam.
Baadhi ya Wananchi wamepora Silaha na wanazitumia kujibu mashambulizi
ya Jeshi la Polisi (habari haijathibitishwa rasmi)
Jengo la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto.
Nyumba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, (Tamisemi), Hawa Ghasia yachomwa moto.
Lodge/Hotel (Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia
Askari wa Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation
inayoendelea imechomwa moto.
Milio ya risasi na mabomu ndicho kinachosikika.
Nyumba kadhaa za watumishi wa Serikali zimechomwa maeneo ya Shangani.
(habari haijathibitishwa rasmi)
Ni magari ya FFU ndio yaliyopo barabarani nayo yanapata
wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo makubwa yaliyowekwa na Wananchi.
Askari kadhaa wamekufa (habari hii haijathibitishwa rasmi)
Baadhi ya watu kadhaa wamechukuliwa na askari kwakuwa
wamepita jirani na gari yao.
Yadaiwa askari wengi waliokuja si wa Mtwara, wengi wametoka
Masasi na Lindi.
Ving'ora vinalia hovyo. Watoto wamefungiwa mashuleni walimu
wamekimbia.
Vituo vya Redio vya Mtwara havizungumzii hali hii ya hatari
bali vinapiga Muziki pengine vinakusanya matukio na habari ya majanga haya ili
Wananchi wayapate.
Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara, mpaka
sasa takriban mabomu 20 na ushee yameshapigwa.
Wakati waziri wa Nishati akisoma hotuba yake kwa hisia kali
na mbwembwe na kusema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar Kauli
mbiu ya Wananchi wa Mtwara ni "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni"
Wananchi walalamikia kituo cha Television na Radio TBC
kuzuia na kukata mawimbi yake kutoonekana wala kusikika katika Mkoa wa Mtwara kwa
muda. Hatimaye hivi Punde matangazo yarejea.
Hili linaendelea wakati bajeti ya nishati na madini
ikiendelea kujadiliwa muda huu Bungeni.
No comments:
Post a Comment