Inapofikia wakati unapohangaika kusoma maandishi madogo yanayotoa maelekezo ya mapishi au unapohangaika kusoma ujumbe kwenye simu yako ya mkononi na ukalazimika kusoma, huku simu ukiwa umeishika ukiielekezea mbali na macho ili uweze kusoma vizuri.
Ni wakati wa kutambua kuwa unahitaji kufanyia kazi tatizo hilo, ikimaanisha kumuona mtaalam wa macho au kununua miwani kwa mkemia au duka la miwani kwa ajili ya kusoma.
Lakini itakuwaje kama hakuna namna ya kupata usaidizi?
Madhara yake yangekuwaje kama kusingekuwa na wataalam wa macho au kutokuwepo kwa miwani zenye gharama nafuu, na ukakubali tu kushindwa kusoma?
Inakadiriwa kuwa watu bilioni 2.5 duniani wanahitaji miwani lakini hawamudu kuzinunua.Takriban asilimia 80 ya hawa wote wako kwenye nchi 20 zinazoendelea hasa Afrika na Asia.
Uonaji hafifu katika nchi masikini, ni kikwazo cha elimu na ajira. Husababisha familia kuwa masikini imeeleza ripoti hiyo.
Taasisi ya ODI Think tank inatahadharisha kuwa wakati bajeti ya misaada inatolewa kwa dharura, kama vile maradhi yanayohatarisha maisha, tatizo la uoni hafifu linapewa umuhimu mdogo na jamii ya kimataifa
Lakini hali ya kushindwa kuona vizuri wakati wa kusoma, na kutokuwa na miwani, ''kunaweza kusababisha watoto kuwa na maisha ya dhiki imeeleza ripoti ya ODI
Hutazamwa kama wasio na mafanikio makubwa au watu walioshindwa, kuliko kutazamwa kama wenye tatizo ambalo lingeweza kufanyiwa kazi.
Miongoni mwa watu wazima, watafiti wanasema, matatizo ya kutoona yana maanisha kukosa fursa katika kazi na kupoteza kipato na kwa uchumi wa kawaida, kupungua kwa uzalishaji.
Ripoti hiyo iliratibiwa na mfanyabiashara wa Hong Kong na mwenye kusaidia watu James Chen, ambaye ameboresha huduma ya afya ya macho jambo la kujitoa yeye mwenyewe.
Alifadhili mradi huo nchini Rwanda, ulioitwa Vision for a Nation, mfuko huo ulikuwa ukitoa huduma ya matibabu ya macho kwa idadi kubwa ya watu.
Wauguzi wamefunzwa kufanya vipimo vya macho, miwani zimekuwa kitolewa kwa bei ya chini au kutolewa bure, kumekuwa na matibabu kwa baadhi ya matatizo ya macho, kama vile dawa za macho za matone.
Mradi wa Rwanda umewafikia watu milioni mbili na umetoa miwani 160,000.
Mfuko wa Bwana Chen, unashawishi suala matatizo ya macho kupewa uzito na kufanya miwani kupatikana wakati wote.
''Miwani zimekuwa zikitengenezwa sehemu mbalimbali duniani kwa takriban miaka 700, lakini kiasi cha theluthi hawawezi kumudu kuwa na miwani''.Ameeleza Chen.
''Wengi wana matatizo ambayo yanaweza kupatiwa ufumbuzi kama kutoona mbali na kutoona karibu, gharama ni kubwa mno , hugharimu dunia matrilioni ya fedha kila mwaka."
Amezitaka serikali za nchi za jumuiya ya madola, zitakazokutana mwezi Aprili, kutoa kipaumbele kwa matatizo ya macho na upatikanaji wa miwani, kwenye miradi ya maendeleo.
Chen amesema kuna namna iliyo rahisi ya kuboresha maisha ya kila mmoja na kuleta faida kwa uchumi wa taifa kwa kuwafanya watu waweze kuzalisha.
Ameeleza kuwa ndani ya nchi za jumuiya ya madola, kufanya miwani zipatikane kunamaanisha uchumi utaimarika na kufikia dola bilioni 44 kwa mwaka.
Elizabeth Stuart mtaalam kutoka Think Tank amesema kuondokana na tatizo hilo kutaimarisha Elimu na kuondoa umasikini.
No comments:
Post a Comment