Thursday, April 26

Upandikizaji maalum wa ngozi unauwezo wa kukabiliana na saratani

Kipandikizi hicho husababisha alama kwenye ngozi iwapo viwango vikubwa vya madini ya Calcium yanapobainika.Haki miliki ya pichaETH ZURICH
Image captionKipandikizi hicho husababisha alama kwenye ngozi iwapo viwango vikubwa vya madini ya Calcium yanapobainika.
Wanasayansi wamebuni kifaa cha kupandikizwa kwenye ngozi ambacho wanasema siku moja kitaweza kutumika kusaidia kubaini saratani zilizomaarufu.
Upandikizi huo unafanya kazi kwa kuchunguza kiwango cha madini ya Calcium kwenye damu, ambayo inahusishwa na saratani kadhaa.
Iwapo kiwango cha Calcium kinapopita kiwango kinachostahili , kipandikizi hicho hutoa tahadhari na kuifanya ngozi hiyo kufura duara dogo lenye rangi ya kahawia.
Wanasayansi wamesema tecknolojia hiyo inaweza kutabiri saratani mapema, lakini wataalam wanasema utafiti huo bado uko katika ''siku zake za mwanzo''
Kwa utafiti huo, uliochapishwa kwenye jarida la kisayansi la Science Translational, watafiti hao walitumia seli za mwanadamu kubaini iwapo mtu ana kiwango kikubwa cha Calcium- ambayo inahusishwa na saratani nne maarufu- saratani ya matiti, tezi dume,figo na hata kufeli kwa figo.
Seli hizo pia zilibuniwa kutoa rangi ya mwili -melanin -alama nyeusi kwenye ngozi, nwyele na macho- iwapo viwango vya calcium vikigundulika kuongezeka kupita kiasi.
Seli hizo zilipandikizwa kwenye ngozi ya panya wawili - mmoja alikuwa na uvimbe wa saratani unaosababisha ongezeko la calcium nyingi na mwengine alikuwa na uvimbe ambao hauathiri viwango vya calcium kwenye viwango vya damu.
Alama hizo ama 'chale' zilionekana kwa panya ambaye ngozi yake ilikuwa na Calcium nyingi, utafiti huo ulibaini hivyo.
Kipandikizo hicho pia kilifanikiwa kilipojaribia kwa ngozi ya nguruwe.
Ikitumiwa kwa binadamu,chale hizo zitakuwa dhihirisho la kumtembelea daktari kwa uchunguzi zaidi , watafiti wamesema.
Wameongeza kwamba kubainika kwa mapema kwa ugonjwa wa saratani unaweza kuwa wakati mwafaka wa kuutibu ugonjwa huo.
Profesa Martin Fussenegger, wa kitengo cha wanasayansi wa ETH huko Zurich,Basel waliongoza utafiti huo wamesema: ''Ugonjwa huo unapojulikana unaongeza nafasi za mtu kuendelea kuishi.''
PanyaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionPanya
''Siku hizi, watu huenda kwa daktari pale uvimbe unapoanza kuleta matatizo. Na kwa wakati huo tayari ni kuchelewa.''
Kipandikizo hicho kinaweza kufanyiwa marekebisho ila alama hiyo ionekane vyema kwenye mwanga mwekundu, watafiti wamesema.
Prof Fussenegger, amesema teknolojia hiyo pia itatumika kwa magonjwa mengine kama ya ubongo - kwa kutafuta alama hizo kwenye mwili na sio kuangazia viwango vya calcium.

'Hapo awali'

Dkt Catherine Pickworth kutoka kituo cha utafiti cha Saratani nchini Uingereza, amesema ''tecknolojia hiyo ya kuvaliwa' ilifanyiwa uchunguzi ni ya 'kusisismua' lakini utafiti huo bado uko katika ''hatua za mapema''.
Alisema :Utafiti huu wa panya umeonyesha kwamba chale za kisaynsi zinauwezo wa kubaini mabadiliko kwa kiwango cha madini ya Calcium kwenye damu , lakini tunahitaji kufahamu iwapo ni ukweli kwa binadamu.
''Viwango vikubwa vya Calcium vinaweza kuwa kielelezo kikuu cha saratani lakini pia kwa magonjwa mengine, kwa hivyo utafiti huu siku moja unaweza kuwasaidia madaktari kubaini iwapo mgonjwa anaweza kufaidika kwa kufanyiwa uchunguzi zaidi.
''Ubainishaji wa saratani mapema ni mojawepo na njia ya kuokoa maisha ya binadamu , kwa hivyo kupata njia bora ya kuwakinga watu ambao wako katika hatari zaidi , au ambao wanaupungufu ni changamoto muhimu.''

No comments:

Post a Comment