Mpasuko huo umekuja kufuatia kuwepo baadhi ya mastaa wanaoona Wema amestahili tuzo hiyo huku wengine wakiamini amepewa kwa upendeleo.
Maneno yalianza kwenye mitandao muda mfupi baada ya Wema kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo aliyokuwa akiwania na Riyama Ally na wasanii wengine wa kike chipukizi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwigizaji Irene Uwoya aliweka picha ya Gabo na kuandika, "Hapa hawajapepesa umestahili."
Mwigizaji Youbnesh maarufu Batuli akaweka picha hiyo hiyo na kuandika," Ukisikia mtu kutenda haki na kutendewa haki ndio hii. Gabo wangu Mwenyezi Mungu aendelee kukunyanyua juu Inshallah, endelea kutunza heshima na tamaduni zetu, keep working hard baba hongera sana."
Kauli hizo zimeonekana kuwakera mashabiki wengi wa Wema na kujikuta wakiwashambulia mastaa hao kwamba kumpongeza Gabo peke yake kunaashiria kuwa hawakubaliani na ushindi wa mwigizaji huyo wa kike aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006.
Pamona na mashabiki kuja juu, mwigizaji Eshe Buheti alikuwa na maoni tofauti na wenzake akionyesha kuamini kuwa Wema alistahili tuzo hiyo.
Hakuishia hapo Eshe aliwatupia lawama mastaa wa Bongo Movie kwa kudharau walipotakiwa kuwasilisha filamu ili zishindanishwe kwenye tuzo hizo.
"Mlitegemea nini wakati tulipoambiwa tupeleke filamu tulilegeza kamba, wenzetu wakatumia fursa. Hili ni funzo tumelipata nadhani mwakani kila mtu ataamka alipolala. Tuache maneno jamani, tupongezane kwa waliostahili.”
Mwingine aliyemtetea Wema ni mwigizaji Faiza Ally akisema waigizaji wana roho mbaya kwamba hawapendi kuona mwenzao akifanikiwa.
No comments:
Post a Comment