Rais Trump amesema kuwa hakufahamu kuhusu malipo ya fedha za Kimarekani 130,000 yaliyolipwa na wakili wakili kwa mchezaji filamu za utupu Stormy Daniel kabla ya uchaguzi wa 2016.
Hii ni mara yake ya kwanza kuzungumzia swala hilo.
Alipoulizwa alipokuwa kwenye ndege ya Air Force One kama alifahamu kuhusu malipo hao na hela zilipotoka , Bwana Trump alisema "Hapana"
Alipoulizwa kwa nini wakili wake Michael Cohen alifanya malipo hayo, Bwana Trump alisema: "Inabidi umuulize Michael"
Muigizaji huyo anasema alifanya tendo la ndoa na Bwana Trump mwaka 2006. Bwana Trump amekana madai hayo.
Bi Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford,anasema alisaini makubaliano ya kubaki kimya kuhusu mashusiano yake na Bw Trump na kulipwa dola za Marekani 130,000 mwezi Oktoba 2016, kabla ya uchaguzi wa urais.
- Mwigizaji adai alitishiwa kuhusu madai ya kufanya ngono na Trump
- Je Trump alikuwa na 'uhusiano' na nyota wa filamu za ngono?
Bi Daniels, ameiambia vyombo vya habari vya Marekani kuwa alitishiwa mwaka 2011 na mtu ambaye hakumfahamu aliye wambia "kumwacha Trump"
Mawakili wa Bw Trump wanataka kulipwa fidia ya $20m (£14m) na mwanamke huyo, wakisema alikiuka makubaliano ya kuweka siri ambayo aliyatia saini katika ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.
Mwanamke anayemtishia Donald Trump
Mwanamke huyo anasema madai hayo hayana msingi.
Stormy Daniels ni nani?
Stormy Daniels alizaliwa Stephanie Clifford, Louisiana mwaka 1979.
Alihamia kwenye soko la kucheza filamu za utupu kwanza kama mtumbuizaji, kabla ya hapo mwaka 2004 alikuwa akiongoza na kuandika filamu.
Obama: Sitanyamaza utawala wa Trump
Jina lake la jukwaani,Stormy Daniels, limetokana na jina la binti wa mwanamuziki wa kundi la Mötley Crüe, 'Storm' na jina la kinywaji aina ya Whisky , 'Jack Danniels'.
Unaweza kumtambua kwenye filamu ya 'The 40-Year-Old Virgin' na 'Knocked Up' na video ya muziki wa kundi la Maroon Five 'Wake up call' .
Mwaka 2010 alifikiria kugombea uongozi kwa nafasi ya useneti Louisiana lakini aliahirisha baada ya kusema kuwa ushiriki wake hautiliwi maanani.
No comments:
Post a Comment