Thursday, April 26

Trump, Macron watafuta muwafaka, wathibitisha ushirikiano wao

Rais Donald Trump na mkewe Melania akiwa na mgeni wake Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mkewe Brigitte wakati walipowasili White House kuhudhuria chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa heshima yao Jumanne, Aprili 24, 2018.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anahitimisha ziara yake ya kwanza ya kiserikali nchini Marekani Jumatano akihutubia mkutano wa pamoja wa Bunge la Marekani na mkutano na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Georgetown.
Wakati wa ziara hiyo ya siku tatu, Macron na Rais wa Marekani Donald Trump walizungumzia ushirikiano wa kibiashara, mazingira, Iran na Syria.
Kwa mujibu wa mwandishi wa VOA viongozi hao wawili walikuwepa kuzungumzia tofauti zao na kusisitiza mahusiano ya karibu yaliyoko kati ya nchi hizo na urafiki wao binafsi.
Wakati wakionyesha urafiki wao kwa maneno na vitendo, Trump na Macron wamekiri kuwa wanashirikiana kuondoa tofauti zao katika mambo kama vile mabadiliko ya hali ya hewa na makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa na Iran.

Rais Trump alisema: “ Haya ni makubaliano yaliyokuwa na msingi mbovu. Ni makubalian mabaya. Ni muundo mbaya. Unashindikana, ulitakiwa usifanyike kabisa. Ninalilaumu Bunge la Marekani. Nawalaumu watu wengi kwa hili. Lakini ilitakiwa makubaliano haya yasiwepo kabisa. Lakini tutaangalia kile kitakachotokea tarehe 12.”
Trump amesema kuwa hatapitisha tena makubaliano hayo ifikapo Mei 12 ambapo ndio wakati wa kutia tena saini hadi pale “utapobadilishwa” na kuingizwa makubaliano mapya yanayoilazimisha Iran kusitisha programu yake ya makombora ya balistika na kuingilia kati masuala ya eneo la Mashariki ya Kati. Macron kwa upande wake amekubali kuwa masuala hayo yanahitaji kushughulikiwa hapo siku za usoni.
Macron amefafanua kuwa: “ Hilo ndio hasa analosema Rais Trump. Sisi tumefikia makubaliano ya nyuklia (na Iran) ya muda mfupi. Na tunayo masuala ya nyuklia ya muda mrefu. Tuna pia suala la utengenezaji wa silaha za balistika. Tunalo pia suala la Iran kuwepo katika eneo. Tunataka kutafuta ufumbuzi juu ya hali hii.”

No comments:

Post a Comment