Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora,Wilbroad Mutafungwa, amesema leo Aprili 9 kwamba wakongo hao waliokamatwa wamo pia watoto chini ya umri wa miaka mitano, vijana na wanawake.
Amesema kuwa Wakongo hao, wamesema kwamba wanatoka mkoa wa Uvilla ambao kuna mapigano wakidai baadhi ya ndugu zao wameuawa.
Amesema wamefika Tabora kutokea Kongo,wakipita mkoa wa Kigoma na wilayani Kahama mkoani Shinyanga na kuwasili Tabora huku mipango yao ikiwa ni kwenda mkoani Mbeya na hatimaye nchini Malawi.
Kamanda Mutafungwa amesema wakongo hao,wanadai kambi za wakimbizi Kigoma hazipokei wakimbizi kutoka Kongo na wao kuamua kwenda Malawi.
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Tabora,wametaka ulinzi zaidi uongezwe mipakani ili kuwadhibiti watu wanaoingia nchini kinyume cha sheria.
"Kama usalama ukiwepo maeneo ya mipakani,watu kama hawa watakuwa wakidhibitiwa kabla hawajaingia nchini"Amesema Hamimu Said mkazi wa Tukutuku Manispaa ya Tabora.
Mkazi wa mtaa wa Rehani,Maulid Hussein,alisema kama watu hao wanataka kudhibitiwa wasiingie nchini ni kumaliza matatizo kwenye nchi zao.
"Endapo tutahakikisha mazungumzo ya amani yanafanyika na makubaliano kufikiwa,tutakuwa tumetatua changamoto hiyo’’amesema
Mkoa wa Tabora umekuwa ukiwakamata wahamiaji haramu mara kwa mara toka nchi jirani hasa Burundi na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kufikishwa mahakamani,ambapo wengine wamefungwa, kulipa faini na kurudishwa makwao.
No comments:
Post a Comment