Filamu kutoka katika kitovu cha utengenezaji filamu duniani Hollywood zimekuwa zikichujwa nchini Saudi Arabia wakati ufalme ukiruhusu urushwaji filamu baada ya miaka thelathini na tano ya marufuku.
Kuonyeshwa kwa filamu ya blockbuster, "Black Panther" ni sehemu ya majaribio ya mapitio ya filamu zinazopitia mchujo kabla ya majumba ya kuonesha filamu kuruhusiwa kuwaonesha waja, awali kila mtu alikuwa akitazama nyumbani kwake, ila kwa hadhira sasa ni rasmi tangu tarehe 18, April mwaka huu .
Maafisa wa serikali, wanadiplomasia na jamii wanatarajiwa kushiriki. Marufuku ya kuoneshwa filamu nchini humo lengo lilikuwa ni kulinda imani ya kihafidhina ya kiislamu pamoja na mila za kitamaduni za nchi hiyo.
Lakini kurudi kwa maonesho ya filamu nchini humo inaelezwa kuwa ni sehemu ya mfululizo wa mabadiliko ya kijamii yenye uhuru unaoingizwa na mwanamfalme Mohammed bin Salman.
No comments:
Post a Comment