China imeongeza ushuru kwa asilimia 25 kwenye bidhaa tofauti kutoka Marekani ikiwemo nyama ya nguruwe, matunda na bidhaa nyingine, zikiwa na thamani ya dola za marekani billioni 3.
Hatua hiyo ya China ambayo imeanza kutekelezwa Jumatatu hii ilitangazwa Jumapili na Wizara ya Fedha ya China, kama jibu dhidi ya hatua ya Marekani kuweka ushuru kwenye chuma na aliminium kutoka China.
Wizara ya Biashara ya China imefahamisha pia kwamba haitotekeleza baadhi ya vipengele vya mkataba wa kimataifa wa biashara ambapo China ilikuwa imekubali kupunguza ushuru kwenye bidhaa 120 kutoka Marekani.
Bali China imesema itaongeza ushuru kwa asilimia 15 kwenye bidhaa hizo za Marekani. Wachambuzi wa masuala ya kiuchumi wanahofia vita hivyo vya kibiashara kati ya mataifa hayo mawili vitaathiri uchumi wa dunia siku za mbele.
No comments:
Post a Comment