Tafiti zinaonyesha kuwa wanawake wana uwezekano mkubwa kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi zaidi ya wanaume.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa asilimia 80 ya watu wanaolazimika kuhama makazi yao kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ni wanawake.
Majukumu yao kama walezi na wanao hudumia familia kwa karibu zaidi huwafanya kuwa katika mazingira hatari zaidi wakati wa mafuriko na ukame unapotokea.
Makubaliano ya mjini Paris mwaka 2015 yaliweka kipaumbele maalum cha kuwawezesha na kutambua kwamba wanawake huathiriwa kwa kiasi kikubwa zaidi katika jamii kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.
Afrika ya kati, eneo ambalo ziwa Chad limetoweka kwa asilimia 90, hali inayolazimu wenyeji wa eneo hilo kuhama na kuwa katika mazingira hatari.
Kila wakati ziwa linapopungua ,wanawake wanalazimika kutembea kwa muda mrefu kutafuta makazi mapya.
Wakati wa kiangazi wanaume wanaenda mjini na kuwaacha wanawake vijijini kuangalia jumuiya. Hivyo wanawake wanalazimikia kufanya kazi zaidi ili kutunza watoto bila msaada wowote.
Lakini sio wanawake wa maeneo ya vijijini peke yake ndio wanaathirika.
Duniani kote wanawake wanaathirika zaidi kutokana na umaskini na kutokuwa na uwezo mkubwa zaidi ya wanaume katika masuala ya kiuchumi hivyo hali ambayo huwafanya washindwe kujikwamua kutoka katika majanga ambayo yanaharibu miundombinu ,ajira na makazi yao.
Aidha zaidi ya nusu ya familia zinazo ishi mjini zinatunzwa na wanawake.
Wakati Katrina ilipotokea mwaka 2005,wanawake na watoto ndio waliathirika zaidi katika upande wa makazi ,afya na hata walikumbana na unyanyasaji wa kijinsia kama kubakwa.
Vile vile mabadiliko ya tabia nchi huathiri shughuli za kibinadamu, athari za hali ya hewa na maafa yanayotokea katika jamii husika huwa na athari tofauti kwa wanawake na wanaume.
No comments:
Post a Comment