Wabunge wa Kenya siku ya Jumanne walizungumzia kuhusu vile ambavyo wamekuwa wakihangaishwa na wahalifu wa mtandaoni wanaotaka fedha mbali na kuwatumia picha za utupu.
Kiongozi wa walio wengi bungeni Aden Duale na mbunge wa Kiminini Chris Wamalwa waliambia bunge vile ambavyo mwanamke mmoja ambaye hawakumtaja jina amewafanya kuhofia kutumia simu zao hadharani kwa kuwa amekuwa akiwatumia picha za utupu.
''Kuna mwanamke ambaye ana nambari za simu za wabunge wote na hututumia picha za utupu mara kwa mara'', alisema Duale.
''Swala hili ni muhimu sana kwa sababu limevunja familia nyingi na ni sharti likabiliwe'', alisema Wamalwa.
- Picha za Utupu
Mbunge huyo wa Kiminini alitaja vile siku moja alipopokea picha za utupu akiwa ameketi na mbunge mmoja mwanamke bungeni na alipozifungua alihisi aibu kubwa.
- Maajabu ya viumbe wenye vichwa viwili
- Mtandao unaowasaidia wasichana kulinganisha uke wao
- Kiongozi wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo atoweka
Kiongozi wa wachache bungeni Junet Mohamed alisema kuwa wabunge wanaume wamekuwa wakihangaishwa na wahalifu wa mitandaoni zaidi ya wenzao wa kike.
''Nimepokea picha za utupu katika simu yangu ambazo ni chafu kuangalia. Picha hizi ni hatari hali ya kwamba unaomba kwamba zisitumwe wakati unapokuwa na familia ama wakati mtoto anapochukua simu yako'',alisema.
''Tatizo kubwa tunalokumbana nalo ni uhalifu wa mtandaoni. Tumehangaishwa, kutongozwa huku kazi za wanasiasa wengine zikiisha kutokana na uhalifu wa mtandaoni''.
- Kutongozwa mtandaoni.
Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Baringo Kaptuya Cheboiwo alisema kuwa sio wabunge wanaume pekee ambao wamekuwa wakinyanyaswa lakini pia wanawake, wengine wao wakitongozwa mtandaoni.
''Wabunge wanaume wanadhani wanatongozwa pekee yao hata sisi tunatongozwa kila mahala'', alisema. Ukiwa na mume ambaye hawezi kuhimili uzito wa tatizo hilo huenda ukapewa talaka''., bi Cheboiwo aliongezea.
Swala hilo liliwasilishwa bungeni na mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Muranga Sabina Chege ambaye alitoa taarifa bungeni akilalamika kuhusu vile walaghai walivyosajili nambari za simu za wabunge na kuzitumia kupata fedha kutoka kwa wananchi wasio na hatia.
Bi Chege alisema kuwa watu hao wamekuwa wakiwalenga wabunge ambao wamefiliwa na wapendwa wao ama wanaotafuta michango ya fedha huku wakituma ujumbe kwa wabunge wengine wakidai kwamba wenzao wanahitaji mchango wao wa kifedha.
Wabunge hao wamemtaka inspekta jenerali wa polisi kufika mbele yao katika kipindi cha siku saba zijazo ili kuelezea njia anazotumia kukabiliana na tatizo hilo la mtandaoni.
- Fedha
''Simu zinazotumiwa huwa zimesajiliwa kwa kutumia majina ya waathiriwa na wabunge wanaolengwa, hawatakuwa na wasiwasi, wakiwa na nia ya kuwasaidia wenzao watakubali na kutuma fedha kama walivyotakiwa'', alisema bi Sabina.
Kiongozi wa wengi bungeni Adan Duale amekuwa akimshutumu mwanablogu mmoja kwa kufungua akaunti ya mtandao wa kijamii kwa kutumia picha yake ili kupata fedha kutoka kwa watu wengine.
''Bloga huyo amekuwa akijipatia fedha kwa kutumia jina langu akiwadanganya watu kwamba amekuwa akitoa kazi na kwamba raia wanapaswa kutoa fedha ili kupokea fursa hiyo'', alisema.
Kiongozi wa wachache bungeni John Mbadi alilaumu kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana kama sababu ya ongezeko la wahalifu wa mtandaoni.
No comments:
Post a Comment