Urusi inatazamia kuwafukuza wanadiplomasia 23 wa Uingereza kutokana na mvutano uliosababishwa na kushambuliwa kwa mpelelezi wa zamani wa Urusi na binti yake nchini Uingereza.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi alisema wafanyakazi kutoka ubalozi wa Uingereza nchini Moscow wanatakiwa kuondoshwa ndani ya wiki moja.
Pia amesema ni lazima ofisi za serikali ya Uingereza nchini Urusi zinazotangaza mahusiano ya kiutamaduni kati ya nchi hizo mbili zifungwe ikiwa ni pamoja na ubalozi wa uingereza huko St.Petersburg.
Hatua ya wanadiplomasia hao kutaka kufukuzwa imekuja baada ya Uingereza kuilaumu Urusi kwa tukio lilitokea tarehe 4 mwezi machi na Urusi kukataa kuhusika kumshambulia mpelelezi wa Uingereza na binti yake.
Mpelelezi wa zamani wa Urusi Bw. Sergei Skripal mwenye miaka 66, na binti yake Bi. Yulia Skripal mwenye miaka 33, bado wapo hospital huku hali zao za kiafya zikiwa hazijatengama, baada ya hivi karibuni kukutwa wakiwa na sintofaham kwenye benchi huko Salisbury.
Uingereza imesema watu hao waliwekewa sumu na wakala wa idara inayoungwa mkono na Urusi itwaye Novichok, na Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amesema Moscow ndio inapaswa kulaumiwa.
Waziri wa mambo ya nje Boris Johnson alisema "kuna uwezekano mkubwa kwamba Rais wa Urusi Vladimir Putin ameamuru shambulio hilo la kijeshi".
Huku msemaji wa Bw.Putin ,Dmitry Peskov amesema, " vitisho hivyo ni vya kutisha na si vya kusamehewa."
Balozi wa Uingereza nchini Urusi Laurie Bristow,aliitwa katika ofisi za wizara ya mambo ya nje nchini humo leo ili kutoa ufafanuzi kuhusu vikwazo hivyo kwa Uingereza.
No comments:
Post a Comment