Rais Trump ameandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twittter kuwa makubaliano na Korea Kaskazini yapo kwenye mchakato wa kutekelezeka ,
siku moja baada ya kukubali kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Ingawa mpaka sasa Korea Kaskazini haijatoa tamko lolote.
Aidha Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence amesema uamuzi wa Korea Kaskazini kutaka kukutana na rais wa Marekani Donald Trump unathibitisha kuwa mpango wa kuitenga Korea Kaskazini unafanya kazi.
Hata hivyo makuliano ya mkutano huo wa kihistoria uliwashangaza waangalizi.
Lakini badae ikulu ya white house ya Marekani imesema mkutano huo hauwezi kufanyika mpaka Korea Kaskazini ichukue hatua thabiti kabla ya mkutano wowote.
Mwezi mmoja tu uliopita ,rais Trump na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un walikuwa wana malumbano makali.
Lakini sasa rais Trump amekubali kuhudhuria mkutano huo alioalikwa licha ya kuwa mwaliko huo uliletwa na Korea kusini.
Vyombo vya habari vya Marekani vinataarifu kuwa rais Trump alifanya maamuzi ya kuhudhuria mkutano huo bila kupata ushauri wowote katika utawala wake.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ambaye yuko kwenye ziara yake ya kwanza barani Afrika amethibitisha kuwa maamuzi hayo yalikuwa ya Trump peke yake na yeye hakufahamu lolote juu ya hilo licha ya kuwa walikuwa na mazungumzo kabla ya tangazo hilo kutolewa.
Ingawa ujumbe huo wa kukaribishwa kwa Trump umekuwa unajichanganya kwa kuwa katibu wake Trump Sarah Sander aliwaambia waandishi wa habari kuwa Korea Kaskazini imehaidi kusitisha mpango wake wa nuklia na wamekubali kufanya hivyo kabla ya mkutano huo.
Trump atakuwa kiongozi wa kwanza wa Marekani kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini kama mkutano huo utaafikiwa kwa kuwa hakuna kiongozi wa Marekani aliyewahi kukutana na kiongozi wa Korea kaskazini .
No comments:
Post a Comment