Mabawa amesema amefikia uamuzi wa kuanzisha kampeni hiyo itakayoitwa 'Washa data tetea Ttaifa' baada ya kubaini ongezeko la watu wanaoitumia vibaya mitandao.
Akizungumza leo Machi 17, Mabawa amesema kwa sasa kuna watu wanahamasisha maandamano wakiamini kuwa hawawezi kukamatwa kwa kuwa wamejificha kwenye kivuli cha mitandao.
"Kuna watu hawana nia njema wanataka kuleta maandamano yasiyo na tija, wanawahamisha Watanzania waende barabarani haya yote ni matokeo ya kutokuwa na elimu sahihi ya mitandao," amesema na kuongeza:
“Hili suala nililiona mapema na nikawafuata baadhi ya viongozi ili nifanye kampeni hii lakini wakanipuuza matokeo yake ndiyo haya.”
Akizungumzia maandamano hayo amesema hayana tija na hayawezi kufanikiwa.
"Huwezi kuitisha maandamano kwenye nchi ambayo wanyonge na maskini wanasikilizwa na watawala, wananchi wanatatuliwa shida zao na serikali ni sikivu, nina uhakika hayatafanikiwa.
"Hata hivyo, hatutakiwi kupuuzia kwa kuwa nchi zilizoingia kwenye machafuko ilianza kama hivi taratibu lazima tutafute ufumbuzi na sio mwingine zaidi ya kuwapa elimu wananchi watumie mitandao vizuri,"amesema Mabawa.
Pia, alimuomba Rais John Magufuli kuitumia kauli mbiu ya ‘Washa data, tetea Taifa’ Siku ya Muungano inayotarajiwa kuadhimishwa Aprili 26.
No comments:
Post a Comment