Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania , Abdul Nondo ambaye pia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam aliye ripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha amepatikana akiwa hai eneo la Mafinga mkoani Iringa kusini magharibi mwa nchi hiyo.
Inadaiwa kuwa alijikuta katika eneo hilo baada ya kuzinduka kutoka katika lindi la usingizi na kuwauliza wenyeji wa eneo alilo jikuta kuwa yuko wapi? ambao walimfahamisha kuwa yuko Mafinga mkoani Iringa na kisha akapelekwa kituo cha polisi kilichoko karibu.
Mahojiano yake katika kituo cha Polisi Mafinga eneo alikopatikana yamefanyika na baadaye kupiga simu kwa ndugu zake. Baada ya kupata taarifa ya kupatikana mwanawe, baba mzazi Mussa Mitumba ameomba namba za askari aliyemfanyia mahojiano ili kujua nini kilimpata mwanae ili aweze kujua kama jambo jingine alilowaambia kuhusiana na kutekwa kwake.
- Marekani: Tunasikitishwa na vitendo vya utekaji na ukatili Tanzania
- Tundu Lissu asimama kwa mara ya kwanza
- Siku ya 100: Azory Gwanda yuko wapi?
Alionekana mara ya mwisho mnamo Jumanne katika afisi za shirika hilo eneo la Sinza, Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyokuwa imetolewa na shirikisho la vyuo vikuu nchini humo, Tahliso.
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) ulisema baada ya kuondoka afisi hizo, Bw Nondo alielekea chuoni na kuaga kuwa anaondoka kwenda nyumbani Madale.
Awali kabla ya tukio hilo mwanafunzi huyo alielezea kwamba alikuwa akifuatiliwa mara kadhaa watu asiowatambua na wenye nguo za kiraia wakijitambulisha kama watu wa usalama ambao wamekuwa wakimpatia vitisho.
No comments:
Post a Comment