Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ameshutumu ukuwaji wa kiuchumi wa China barani Afrika wakati akitarajiwa kuanza ziara rasmi katika bara hili hii leo.
Amesema China inahimiza mataifa ya Afrika kuitegemea, na ilitumia rmikataba ya kifisadi na kuhatarisha rasilmali asili za mataifa ya Afrika.
Muda mfupi kabla ya kuondoka kutoka Marekani kwa ziara ya wiki nzima katika nchi ya Chad, Djibouti, Ethiopia Kenya na Nigeria, Tillerson ameahidi msaada wa dola milioni 533 katika ufadhili mpya wa kibinaadamu kwa Somalia, Sudan kusini, Ethiopia, na Chad - kimsingi kugharamia vitu kama chakula, maji na matibabu ya afya.
Amefafanua kuwa maudhui ya ziara yake ni pamoja na kupambana na ugaidi, democrasia, utawala , biashara na uwekezaji.
Baada ya hapo aliishutumu China kwa uwekezaji wake anaoutaja kuwa na uwezo wa kuimarisha miundo mbinu Afrika lakini unoongeza madeni na uliounda nafasi kidogo za ajira.
Katika miaka 20 iliyopita, biashara kati ya Afrika na China imeshamiri kutokana na hamu kubwa iliyonayo China kwa madini ya bara la Afrika.
Hatahivyo makampuni ya ujenzi ya China yamechangia maendeleo makubwa katika miundo mbinu iliysahaulika kwa muda mrefu, zikiwemo barabara, katika baadhi ya mataifa ya Afrika.
Mafao upande mmoja, makato upande mwingine
Rex Tillerson amesema anataka mataifa mengine yanapaswa kuchangia pia katika usaidizi huo na amepongeza mipango ya biashara ya Marekani na Afrika ambayo anasema imesaidia kushinikiza biashara isiyo ya mafuta.
Lakini wachambuzi wana shaka kuhusu manufaa yatakayo tokana na kunyoosha mkono huku. Wengi wanauliza hatua hii ina maana gani?
Ujumbe mkuu wa Rex Tillerson ni kwamba Marekani tofuati na Uchina ndio rafiki wa dhati kwa bara la Afrika.
Msaada aliotangaza kwa mataifa kadhaa ya Afrika yaliotishiwa na baa la njaa bila shaka utakaribishwa, lakini Tillerson anamfanyia kazi rais ambaye mara kwa mara amezungumza kuhusu kupunguza mzigo wa mataifa ya nje kwa Marekani.
Tamko hilo limetolewa katika wakati ambapo kuna uwezekano mkubwa wa kusitishwa ufadhili wa Marekani katika operesheni za kulinda amani na misaada - tena katika wakatiamabpo Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya kati na Sudan kusini miongoni mwa nchi nyingine zimezilemaza operesheni zilizopo za Umoja wa mataifa.
Katika utawala ambao umeng'ang'ana kuidhinisha uwiano katika sera yake ya kigeni , na ambayo inaishi kwa kauli ya Marekani kwanza, itakuwa sio jambo la uhalisi kumtarajia Waziri Tillerson afanye mabadiliko katika uhusiano katiya Marekani na Afrika.
No comments:
Post a Comment