Saturday, March 31

Kasisi wa Msumbiji akamatwa na polisi kwa kujaribu kumfufua mfu

MsalabaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKasisi huyo alidai kuwa roho mtakatifu alimwambia asafiri hadi katika hospitali ya Chimoio katika jimbo la Manica, kumfufua mfu
Kasisi mmoja nchini Msumbiji amejipata mikononi mwa polisi baada ya kujaribu kumfufua mwanamume mmoja eneo la kati la Msumbiji bila mafanikio
Kasisi huyo alidai kuwa roho mtakatifu alimwambia alisafiri hadi katika hospitali ya Chimoio katika jimbo la Manica, kufanya muujiza huo.
Kasisi huyo ambaye aliyedai kuwa na uwezo wa kufanya mwujiza huo aliweza kuikonga mioyo ya maafisa wa hospitali hadi wakamruhusu aingie ndani ya chumba cha maiti kuutekeleza muujiza wake
Hata hivyo baada ya siku mbili za maombi makali, hakuweza kabisa kurejesha uhai wa marehemu.
Haikuishangaza familia ya marehemu.
Dada yake marehemu - ambaye hakutaka jina lake litajwe - aliwaambia waandishi wa habari:
"Kasisi aliomba, akaomba na kuomba hadi akanena kwa lugha. Alizungusha kichwa cha marehemu huku na kule huku akiomba.
"Lakini hakuna hata sehemu ya marehemu kaka yangu iliyoweza kutikisika. Wakati mmoja kasisi alipaza sauti akisema: 'amka, kijana wa Mungu!"
"Hatukuamini kasisi angefanya mwujiza wowote. Hii ni kwa sababu hakuwahi, hata wakati mmoja, kuthibitisha uwezo wake wa kumrejeshea mfu uhai wake.
"Tangu wakati huo kasisi alikamatwa na yuko mikononi mwa polisi akishtakiwa kwa kosa la kumkosea heshima mfu."

No comments:

Post a Comment