Saturday, March 31

Felix Tshisekedi achaguliwa na upinzani kugombea urais DRC

Felix Tshisekedi (
Image captionFelix Tshisekedi (pichani) ni mwana wa waziri mkuu wa zamani na muasisi wa muungano wa upinzani wa UPDS -Etienne Tshisekedi, aliyefariki dunia mjini Brussels mwezi wa February mwaka jana
Chama kikuu cha upinzani kimemchagua leo (Jumamosi) mwanae muasisi wa chama hicho Felix Tshisekedi kama mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Muungano huo wa pinzani UDPS unasema Felix Tshisekedi, mwana wa waziri mkuu wa zamani wa taifa hilo Etienne Tshisekedi, aliyefariki dunia mjini Brussels mwezi wa February mwaka jana, ndiye atakayekuwa mgombea wake katika uchaguzi wa mwezi Disemba.
Uchaguzi wake umefanyika baada ya mkutano wa wajumbe wa chama hicho uliofanyika usiku kucha katika mji mkuu Kinshasa.
Etienne Tshisekedi alifahamika sana kama kiongozi maarufu wa upinzani tangu enzi za utawala wa dikteta Mobutu Seseseko
Image captionMuasisi wa muungano wa upinzani wa UPDS -Etienne Tshiseked (pichani) ndiye baba yake Felix Tshiseked
Tshisekedi pia amechaguliwa kuongoza chama kwa idadi kubwa ya kura...akijizolea kura 790 kati ya 803 za wajumbe wa chama.
"Nina imanikwamba UDPS itaingia madarakani mwaka huu kuweka mambo sawa nchini''
" alisema Tshisekedi
Uchaguzi wa rais nchini DRC unatarajiwa kufanyika tarehe 23 Disemba baada ya kuahirishwa mara mbili, jambo lililosababisha ghasia zilizohofiwa kuliingiza taifa hilo vitani.
Maandamano ya upinzani DRC dhidi ya rais Joseph Kabila yalisababisha vifo vya makumi kadhaa ya watu
Image captionMaandamano ya upinzani DRC: Ghasia za maandamano ya upinzani za kumtaka rais Joseph Kabila aondoke madarakani zinakadiriwa kuwauwa makumi kadhaa ya watu
Rais Joseph Kabila amekuwa madarakani tangu mwaka 2001 na alitakiwa kuondoka madarakani mwishoni mwa mwaka 2016 baada ya kumaliza mihula yake miwili inayokubalika kikatiba.
Hofu juu ya hatma ya rais Kabila mamlakani ilitawala miongoni mwa raia walioanzisha maandamano yaliyokabiliwa na mashambulio ya vikosi vya serikali pamoja na kukamatwa kwa waandamanaji.
Ghasia za maandamano ya upinzani zinakadiriwa kuwauwa makumi kadhaa ya watu.
kulingana na matokeo ya kura ya maoni yaliyotangazwa Ijumaa, asilimia 69 ya raia hawana imani kwamba tume ya uchaguzi nchini humo inaweza kuendesha uchaguzi wa haki na asilimia 80 wana maoni hasi juu ya kabila.
Rais wa DRC Joseph Kabila
Image captionRais Joseph Kabila alitakiwa kuondoka madarakani mwishoni mwa mwaka 2016 baada ya kumaliza mihula yake miwili inayokubalika kikatiba, jambo lililopingwa vikali na upinzani
Asilimia 66 wangependelea kumchagua mgombea wa upinzani na kabila angepata asilimia sita tu iwapo angetaka kugombea tena urais
Muungano wa upinzani UDPS wulianzishwa mnamo mwaka 1982 wakati wa utawala wa dikteta Mobutu Sese seko.
Umekuwa katika upinzani tangu wakati huo na umekuwa ukitawaliwa na mgawanyiko miongoni mwa wanachama wake.

No comments:

Post a Comment