Wednesday, December 6

Unaisikia sauti katika video hii?

A still from the skipping pylon gifHaki miliki ya picha@IAMHAPPYTOAST
Image captiongif hii iliundwa na @IamHappyToast mwaka 2008
Umeitazama gif hii mtandaoni? Je, uliisikia ikitoa sauti yoyote?
Kuna baadhi ya watu wanaosema wanaweza kuisikia sauti boriti hizi zinapogonga chini na kwamba picha hii ina mtetemo.
Gif hii iliundwa na @IamHappyToast mwaka 2008 kama sehemu ya shindano ya photoshop katika b3ta.com na imekuwa ikisambazwa mtandaoni tangu wakati huo.
Baadhi ya watu mtandaoni wamekuwa wakijadili hali hii kwamba baadhi ya watu wanaisikia ikiwa na sauti na wengine hawasikii sauti hata kidogo.
Wengi wameielezea kama "njozi ya masikio" au hata "mazingaombwe kwa masikio".
Ilianza kuzua mjadala wikendi iliyopita tena Dkt Lisa DeBruine kutoka Taasisi ya Sayansi ya Neva na Saikolojia katika Chuo Kikuu cha Glasgow alipowauliza watu wanaomfuata kwenye Twitter waeleze huwa wanahisi nini wakiitazama.
online pollHaki miliki ya picha@LISADEBRUINE/TWITTER
Dkt DeBruine alipokea majibu zaidi ya 245,000, baadhi wakisema walisikia sauti fulani.
Asilimia 70 ya watu walisema walisikia sauti ya mshindo wa kuanguka kwa kitu.
Mtu mmoja anayeugua tatizo la kusikia kelele za ajabu kwenye macho ni mmoja wa waliosema walisikia sauti hiyo ya kishindo. Lakini alisema pia kwamba ilionekana kuzuia kwa muda tatizo lake.
Baadhi ya watu wamejaribu kutoa ufafanuzi kuhusu nini labda kinatokea.
Wanapendekeza kwamba ni mfumo wa neva, ambapo: "Ubonga 'unatarajia/unabashiri' kile kinachofaa kufanyika ukiona picha kama hizo na kutuma ujumbe wa matarajio hayo kwa sehemu ya ubongo inayoangazia sauti. Ndiyo sababu watu wengine huenda hata wakahisi mtetemo."
"Fikira zangu zinaniambia wkamba kutikisika kwa kamera kunasababisha hayo yote. Chochote kinachoweza kutikisa kamera kiasi hicho bila shaka kitasababisha sauti ya kishindo," aliandika mwingine kwenye Twitter.
Aliyeunda gif hiyo anaonekana kuvutiwa na ufafanuzi huo.
Dkt DeBruine aliambia BBC: "Sijui ni kwa nini baadhi ya watu wanaisikia sauti hii kwa ufasaha, wengine wanahisi tu na wengine hawahisi chochote. Baadhi ya watu wasioweza kusikia na wengine wenye matatizo ya kusikia wote nimekumbana nao waliopata hisia zote tatu, sawa na watu wenye tatizo la aphantasia (tatizo la watu kutoweza kufasiri vyema picha kwenye ubongo)."
"Nilifikiri baadhi ya wanasayansi ya macho wangefuatilia hili na kutufafanulia moja kwa moja, lakini yamkini kuna mambo mengi ambayo yanaweza kusababisha hili, na wanasayansi bado hawajaafikiana.

No comments:

Post a Comment