Amesema hali hiyo inasababishwa na uzembe wa maofisa afya ambao hawatekelezi majukumu yao ipasavyo.
Ummy amesema hayo leo Jumatano Desemba 6,2017 alipozungumza na wananchi wa Kijiji cha Humekwa wilayani Chamwino mkoani Dodoma, kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya kitaifa ya usafi wa mazingira kesho Desemba 7,2017.
Ametoa agizo kwa maofisa afya kuzingatia usafi wa mazingira kwa kuwa Tanzania haiwezi kuwa nchi yenye uchumi wa kati ikiwa usafi hautazingatiwa.
"Tunazungumzia kuokoa fedha za Serikali na kuzielekeza kwa jamii kwenye mambo yanayogusa wananchi moja kwa moja. Kwa uchambuzi wa Benki ya Dunia tunapoteza Sh340 bilioni kila mwaka kutokana na kukosekana hali ya usafi," amesema Ummy.
Amesema litakuwa kosa la jinai kwa kaya isiyokuwa na choo bora baada ya sheria kubadilishwa.
No comments:
Post a Comment