Maafisa nchini Marekani wanasema kuwa Rais Trump anatarajiwa kutangaza wiki ijayo kuwa Marekani inatambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel hatua ambayo wakosoaji wanasema kuwa itachochea mzozo zaidi katika eneo hilo.
Hali kamili ya mji huo inakumbwa na utata huku pande zote mbili za Israel na Palestina zikidai kuwa ndio mji wao mkuu.
- Ubalozi wa Marekani kuhamia Jerusalem?
- Israel yafungua eneo takatifu Jerusalem
- Israel kujenga nyumba 560 mashariki mwa Jerusalem
- Viongozi wamsifu Peres mazishi yake Jerusalem
Trump alitoa ahadi ya kampeni ya kuhamisha ubalozi wa Marekani kutoka Tel Aviv hadi Jerusalem.
Mwandishi wa BBC anasema kwa kutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel, Trump anaashiria hatua ya kutekeleza ahadi yake ya kampeni.
No comments:
Post a Comment