Katika jaribio la karibuni zaidi la kombora lenye nguvu zaidi la Korea Kaskazini Marekani imesisitiza kuwa China ionyeshe usimamizi wake na kuchukua hatua kitu ambacho mpaka sasa haijakuwa tayari kufanya- kusitisha kuwapa mafuta Pyongyang.
Wachambuzi wamesema kuwa hiari hiyo bado ni hatua ambayo China inaonekana haiko tayari kuchukua, ni kitu ambacho ingefaa wakafanya hima kulifikiria suala hilo.
“Marekani na China bila shaka wataongeza shinikizo la vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini. Hilo ni jambo halizuiliki na Korea Kaskazini wanastahili kuwekewa vikwazo hivyo, hasa ilivyokuwa kutengeneza kwao kwa kombora la Hwasong-15, limeongeza kiwango cha vitisho kwa jumuiya yay a kimataifa na Marekani,” amesema Zhao Tong, mtafiti katika kituo cha Carnegie Tsinghua kinachoshughulikia sera za dunia.
Zhao amesema linapokuja suala la vikwazo kuna fursa ndogo sana iliyobakia.
“Kuzuia kupeleka mafuta ni kitu China haitoweza kukifanya kwa urahisi. Pengine vikwazo zaidi vinahitaji kuwekwa dhidi ya (North Korea) wafanyakazi (wanaofanya kazi China) au wapigwe marufuku moja kwa moja,” amesema.
China tayari imeagiza kufungwa kwa biashara za Korea Kaskazini nchini humo na kuyataka makampuni ya Kichina kuwa hawatoweza kuajiri wafanyakazi wapya kutoka Kaskazini au mikataba mipya.
Upelekaji wa mafuta umekuwa ni jambo ambalo Beijing inaliendea kwa tahadhari kubwa.
Pia, ni suala ambalo China itabidi walipime kwa uangalifu mkubwa, amesema Jia Qingguo, Professor wa sayansi za kisiasa Peking University.
“Iwapo mafuta yatasitishwa kabisa, inaweza kupelekea matatizo makubwa ya kiuchumi Korea Kaskazini na hata matatizo ya kisiasa. Korea Kaskazini inaweza kugeuka kuwa na machafuko,” amesema.
Kitu cha kwanza ambacho China inawasiwasi juu ya Korea Kaskazini ni utengenezaji wao wa silaha za nyuklia; la pili, vipi inaweza kuepusha machafuko (Katika rasi hiyo) ambayo yanaweza kuleta vita.”
Akizungumza Umoja wa Mataifa Jumatano, Balozi wa Marekani Nikki Haley amesema Washington inategemea kuwa Rais wa China Xi Jinping atachukua msimamo thabiti kuidhibiti Korea Kaskazini.
No comments:
Post a Comment