Mshauri wa maswala ya usalama wa rais Donald Trump amesema kuwa Marekani na washirika wake wako katika harakati kutatua tatizo na Korea Kaskazini kabla ya taifa hilo kuafikia mipango yake ya kinyuklia.
H-R McMaster alikuwa akizungumza katika mkutano wa ulinzi mjini Carlifonia ambapo alionya uwezekano wa vita dhidi ya Korea Kaskazini unaendelea kuongezeka kila uchao.
Hata hivyo aliongezea kuwa kuna njia za kutatua mzozo huo bila ya kutumia vita.
- Korea Kaskazini: Tunaweza kushambulia eneo lolote Marekani
- Trump: Tutaiangamiza Korea Kaskazini iwapo vita vitazuka
- Urusi yadai Marekani inaichokoza Korea Kaskazini
Ameitaka China kuiwekea vikwazo vya mafuta taifa hilo ili kufanya kuwa vigumu kwa Pyongyang kujaza mafuta makombora yanayofanyiwa majaribio.
Korea Kaskazini imeishutumu Marekani kwa kuchochea vita.
Imetaja zoezi la pamoja la kijeshi kati ya Korea kusini na Marekani kuwa la uchochezi na kwamba linaweza kusababisha vita.
No comments:
Post a Comment