Mshauri wa masuala ya usalama wa Ikulu ya White House nchini Marekani, HR McMaster, amesema kuwa Marekani iko mbioni kukabiliana na tishio kutoka Korea Kaskazini
Uwezekano wa kutokea vita unaongezeka kila siku lakini vita sio suluhu pekee, aliuambia mkutano wa ulinzi.
Matamshi yake yanakuja siku tatu bqada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio lake la kwanza la kombora la masafa marefu katika miezi miwili kinyume na vikwazo vya Umoja wa Mataifa.
Kombora hilo lilipaa mbali na makombora mengine ambayo yalijaribiwa awali kbala ya kuanguka katika bahari ya Japan.
HR McMaster ameitaka China kuiwekea vikwazo vya mafuta taifa hilo ili kufanya kuwa vigumu kwa Pyongyang kujaza mafuta makombora yanayofanyiwa majaribio.
Korea Kaskazini imeishutumu Marekani kwa kuchochea vita.
Imetaja zoezi la pamoja la kijeshi kati ya Korea kusini na Marekani kuwa la uchochezi na kwamba linaweza kusababisha vita.
No comments:
Post a Comment