Monday, December 4

Madaktari wafutwa kwa kutangaza kimakosa kuwa mtoto alikuwa amekufa India

NurseHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMadaktari wafutwa kwa kutangaza kimakosa kuwa mtoto alikufa India
Hospitali kwenye mji mkuu wa India, Delhi imewafuta kazi madaktari wawili waliotangaza kimakosa kuwa mtoto aliyekuwa amezaliwa alikuw amekufa.
Madaktari kwenye hospitali ya kibinafsi ya Max, walikuwa wametangaza kuwa mtoto alikuwa amekufa saa kadhaa baada ya pacha wake kuzaliwa akiwa amekufa tarehe 30 Novemba.
Wazazi waligundua kuwa mtoto huyo alikuwa hai wakati wakiwa njiani kwenda kumzika.
Kisa hicho kilizua ghadabu na mjadala kuhusu huduma za hospitali ya kibinafsi ambazo mara nyingi ni ghali mno,
Uchunguzi wa serikali kuhusu kisa hicho unaendelea.
Kisa hicho kilitokea wakati wazazi waligundua kuwa mmoja wa watoto hao alikwa hai ndnai ya mfuko wa plastiki ambao madaktari walikuwa wamemweka.
Kulingana na babu yake mtoto huyo, familia hiyo iliyokuwa imepigwa na mshango na kumkimbiza mtoto huyo hospitalini ambapo waliambiwa kuwa mtoto wao bado alikuwa hai.

No comments:

Post a Comment