Wednesday, December 6

KUBENEA: SIONDOKI CHADEMA LABDA NIFE


Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea leo ameondoa utata wa uvumi wa kuondoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kusema kuwa hana mpango wa kuhamia chama hicho labda awe amefariki.
Amesema hana nia wala dhamira ya kuondoka katika chama hicho kwani amejenga jina lake kwa zaidi ya mika 15 hadi kupata ubunge uwanja ambao ni mpana hawezi kusaliti wananchi wa Ubungo na wengine waliojinyima kwa kumpigania katika safari yake kisiasa.
“Siwezi kuondoka Chadema labda niwe nimekufa au jambo jingine litokee. Kuna watu nimewashawishi kujiunga Chadema akiwamo Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye na Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Lowassa, nina mkono wangu hum oleo niondoke niwaache, watanionaje.
“Kwa kwa uelewa wangu sioni jipya ambalo litanishawishi kujiunga na CCM mimi huwa sinunuliki sijawahi kununuliwa nikifanya jambo lolote lile basi limetoka ndani ya moyo wangu. Kama vishawishi vya fedha nimepitia vingi sana lakini sijawahi kuyumba kwenye msimamo wangu, ahadi za uhondo tumekuwa tukipewa nyingi sana lakini sijawahi kuyumba,” amesema Kubenea.
Amesema hizo ni propaganda za CCM ili wasihojiwe mambo ya msingi yakiwamo Sh milioni 50, na kuongeza kuwa: “Leo hiki chama huwezi jua ni chama cha ujamaa au ubepari. Kinahusbiri kuwa chama cha wanyonge lakini chama cha wanyonge ndicho kilichovunja nyumba za wanyonge kutoka Kimara hadi Kibaha na ndani ya mwezi mmoja wanatakiwa kuhama utafikiri unahamisha tundu la ndege bila kulipa fidia.
“Chama cha wanyonge ndicho kilichoondoa wafanyakazi kwa madai ya vyeti feki na hawapati kiinua mgongo halafu chama hicho hicho kina mtu ambaye hana vyeti anatumia cheti cha mtu na kinamkumbatia mimi nijiunge kwa lipi.”

No comments:

Post a Comment