Wednesday, December 6

Hali ya ghasia nchini DRC ni mbaya kuliko iliyo nchini Syria

Hali iliyosababishwa na ghasia DRC ni mbaya kuliko ya SyriaHaki miliki ya pichaNRC/CHRISTIAN JEPSEN
Image captionHali iliyosababishwa na ghasia DRC ni mbaya kuliko ya Syria
Zaidi ya watu 5,500 walikimbia makwao nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kila siku wakati wa nusu ya kwanza ya mwaka 2017, na kusababisha shirika moja la misaada kutaja hali huyo kuwa mbaya zaidi.
Viwango hivyo vinamaanisha kuwa kwa mwaka wa pili mfululizo, DR Congo ni nchi iliyoathirika vibaya na kuhamia kwa watu kuliosababishwa na mzozo duniani, kwa mujbu wa shirika la Internal Displacement Monitoring Centre (IDMC).
Mapigano kati ya makundi yenye silaha, kuongezea na mzozo wa kisiasa wakati Rais kabila amekataa kuondoka madarakani imefanya hali kuwa mbaya, mkurugenzi wa Norwegian Refugee Council's (NRC) nchini DRC, Ulrika Blom alisema.
"Ni hali mbaya. Idadi ya watu wanaokimbia ghasia ni kubwa kuliko ya nchini Syria, Yemen na Iraq.
Licha ya kuwepo watu milioni 4 wasio na makao na zaid ya watu milioni 7 wanaokumbwa na uhaba wa chakula msaada haijakuwa wa kutosha.
Umoja wa Mataifa ulitangaza ombi lake la juu zaidi mwezi Oktoba, lakini ni chini ya nusu ya pesa zinazohitajika zimepokelewa.

No comments:

Post a Comment