Monday, December 4

Almasi iliyopatikana nchini Sierra Leone kuuzwa mjini New York

Ni almasi ya 14 kwa ukubwa kuwai kupatikana duniani na pia ndiyo kubwa zaidi kuwai kupatikana nchini Sierra Leon tangu mwaka 1972.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNi almasi ya 14 kwa ukubwa kuwai kupatikana duniani na pia ndiyo kubwa zaidi kuwai kupatikana nchini Sierra Leon tangu mwaka 1972.
Almasi ya karati 709 ambayo iligunduliwa na kundi la wachimba migodi nchini Sierra Leone mapema mwaka huu imeuzwa kwenye mnada hii leo mjini New York.
Ni almasi ya 14 kwa ukubwa kuwai kupatikana duniani na pia ndiyo kubwa zaidi kuwahi kupatikana nchini Sierra Leon tangu mwaka 1972.
Jiwe hilo la thamani liligunduliwa na Emmanuel Momoh, mhubiri wa kikiristo kwenye wilaya iliyo mashariki ya Kono
Aliamua kuiuzia serikali badala ya kuwauzia madalali.
Bw. Momoh aliiambia BBC kuwa kwa kuiuza almasi hiyo kwa madalali hakungeinufaisha jamii.
Kuuzwa kwa almasi hiyo kunafanywa na kampuni inalojulikana kama Rapaport.
Mwenyekiti wa kampuni hiyo Martin Rapaport aliiambia BBC kuwa almasi hiyo ni ya kupendeza..
Alisema kuwa mapato kutoka kwa almasi hiyo zinaenda nchini Sierra Leone na kwamba fedha hizo zitasaidia jamii ambapo ilipatikana.

No comments:

Post a Comment