Mwanamume mmoja amelipua maguruneti mawili katika mahakama moja mashariki mwa Ukraine , akijiua pamoja na mmoja wa washukiwa wa mauaji ,kulingana na maafisa wa polisi.
Mlipuko huo ulitokea wakati wa kikao cha kusikizwa kwa kesi hiyo mjini Nikopol katika jimbo la Dnipropetrovsk.
Mtu huyo ni baba ya mmoja wa waathiriwa waliouawa kulingana na maafisa wa polisi.
Takriban watu tisa walijeruhiwa, ikiwemo washtakiwa wawili , walinzi wawili afisa mmoja wa mahakama na raia.
Washtakiwa hao watatu wanatuhumiwa kuifyatulia risasi gari moja na kuwaua abiria wawili mnamo mwezi Februari 2016 akiwemo mwana wa mtu ambaye alilipua vilipuzi hivyo , kulingana na vyombo vya habari.
Kulingana na ripoti za awali mtu mmoja alitoa maguruneti mawili na kuyalipua wakati wa kusikizwa kwa kesi ya mauaji kulingana na mtandao wa Ukrainska Pravda ambao ulimnukuu msemaji wa polisi Yaroslav Trakalo akisema.
Mtu huyo alichukua hatua hiyo baada ya kusikia kwamba kesi hiyo inaahirishwa na kwamba washukiwa wanafungwa mikono.
Uchunguzi sasa umeanzishwa.
Mzozo unaoendelea mashariki mwa Ukraine unamaanisha kwamba kuna umiliki wa silaha miongoni mwa raia.
Zaidi ya watu 10,000 wamefariki katika mzozo huo uliotokea mnamo mwezi Aprili 2014, muda mfupi baada ya Urusi kulinyakua eneo la kusini la rasi ya Crimea.
No comments:
Post a Comment