Thursday, November 30

Wanajeshi 2 wa zamani Argentina wahukumiwa kifungo cha maisha jela

Baadhi ya ndugu wakisikiliza kesi hiyo mjini Buenos Aires siku ya Jumatano
Image captionBaadhi ya ndugu wakisikiliza kesi hiyo mjini Buenos Aires siku ya Jumatano
Maofisa wawili wa zamani wa jeshi la maji la Argentina wamehukumiwa kifungo cha maisha kwa makosa ya ukiukaji wa haki za binadamu, waliyoyatekeleza kati ya mwaka 1976 na 1983 chini ya utawala wa kijeshi.
Kaptain Alfredo Astiz na Jorge Eduardo Acosta walikutwa na hatia ya kuhusika katika mauaji ya mamia ya wanasiasa wa upinzani.
Hawa ni kati ya washitakiwa 54, kati yao raia ni wawili, walioshitakiwa kwa makosa ya ukiukwaji wa haki za binadamu,na mauaji ya mamia ya wanasiasa wa upinzani,katika kituo chao cha mateso cha ESMA.
Ukatili huo ulifanyika,hapo ilikuwa ni shule ya ufundi makenika ya wanamaji hao.
Hatua hii inaatajwa na wemngi kuwa itaifanya Argentina kuheshimika zaidi kimataifa.

No comments:

Post a Comment