Friday, November 3

Wanaharakati wa wanyama wakosoa uchomaji wa kuku Tanzania

KukuHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKuku
Kundi moja la wanaharakati wa haki za wanyama nchini Tanzania limekosoa uchomaji wa kuku 6,400 walioingizwa nchini humo kutoka Kenya kinyume na sheria ili kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa homa ya ndege.
Kuku hao walichomwa na maafisa wa wizara ya mifugo na uvuvi wakishirikiana na maafisa wa usalama baada ya kukamatwa katika mpaka wa Namanga siku ya Jumatatu usiku.
Mkurugenzi wa shirika linalopigania haki za wanyama nchini Tanzania Thomas Kahema amesema kuwa kuna njia nyengine madhubuti za kukabiliana na tatizo kama hilo na ingekuwa bora kuwarudisha kuku hao nchini Kenya badala ya kuwachoma kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania likiongezea kuwa kumekuwa na hisia kali katika mitandao ya kijamii.
Vifaranga wa kuku 6,400 wenye thamani ya zaidi ya dola 5,000 wamechomwa moto Tanzania
''Uamuzi huo umeharibia jina Tanzania kwa majirani zetu'' , alisema bwana Kahema kama alivyonukuliwa.
Uagizaji wa kuku kutoka nje watishia wafugaji Tanzania
Mfanyiabiashara Mary Matia,23, aliwaingiza kuku hao wenye thamani ya $5000 kutoka Kenya na aliangalia kwa uchungu mkubwa na kutoamini wakati vifaranga hao walipochomwa , alisema mwandishi wa BBC Balthazar Nduwayezu kutoka mji wa Namanga.
Tanzania ilipiga marufuku uingizaji wa kuku yapata muongo moja uliopita kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa homa ya ndege katika eneo la Afrika mshariki.

No comments:

Post a Comment