Monday, November 6

Wafikishwa mahakamani wakidaiwa kumshambulia mgombea udiwani


Arusha. Wafuasi 12 wa Chadema mkoani Arusha wanaotuhumiwa kumshambulia mgombea udiwani wa CCM katika Kata ya Muriet, Francis Mbise wamefikishwa mahakamani.
Washtakiwa hao wamefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Maromboso iliyopo jijini Arusha.
Miongoni mwa washtakiwa hao ni Kaimu Katibu wa Chadema Wilaya ya Arusha, Innocent Kisanyage na mwenyekiti wa chama hicho Mtaa wa Mlimani, Yohana Gasper.
Baada ya kufikishwa mahakamani wamepelekwa mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka yanayowakabili.

No comments:

Post a Comment