Rais wa Marekani na Korea Kaskazini wamerejelea vita vyao vya maneno kufuatia mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni wa Korea Kaskazini ilimuita Trump kuwa "mchochezi wa vita na mzee" na kusisitiza kuwa haiwezi kamwe kuachana na mipango yake ya nyuklia.
Rais Trump alijibu kwa kuandika katika mtandao wake wa kijamii wa Tweeter kuwa, anashangaa ni kwa namna gani Kiongozi wa Korea Kaskazini anamuita mzee.
Kwa maneno yake, Bwana Trump alisema kuwa hatamuita Rais Kim Jong-un, kuwa mtu "mfupi na mnene".
Anasema kuwa anajaribu sana kwamba siku moja atakuwa rafiki wake wa karibu.
Trump awali alimkejeli kiongozi huyo mkuu wa Korea Kaskazini, kwa kumuita mwendawazimu na 'mtu wa kuunda zana za roketi'.
No comments:
Post a Comment