Sunday, November 26

Upinzani kuandaa mkutano siku ya kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta

Viongozi wa upinzani wa NASA nchini Kenya wakiongozwa na Raila OdingaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionViongozi wa upinzani wa NASA nchini Kenya wakiongozwa na Raila Odinga
Upinzani nchini Kenya Nasa umesema kuwa utaandaa mkutano sambamba siku ambayo rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa.
Mkutano huo utafanyika katika uwanja wa Jacaranda katika eneo la Embakasi mjini Nairobi.
Kongamano hilo ambalo maafisa wa polisi wanasema sio halali huenda likasababisha makabiliano makali kati ya wafuasi wa upinzani huo na maafisa hao wa polisi
Tayari viongozi wa upinzani wamesema kuwa hawatambui ushindi wa Uhuru Kenyatta kwa madai kwamba uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 26 mwezi Novemba ulikuwa haramu.
Vilevile kiongozi wa muugano huo Musalia Mudavadi amesema kuwa watatumia njia halali zilizopo kupinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta licha ya kuidhinishwa na mahakama ya juu.
Mudavadi pia amewaambia Wakenya kutohudhuri sherehe ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa Kasarani siku ya Jumanne na badala yake kuhudhuri mkutano wa upinzani huo ili kuomboleza mauaji ya waathiriwa waliouawa na maafisa wa polisi.
Mapema katika taarifa na vyombo vya habari kamanda wa polisi mjini Nairobi Japhet Koome alisema kuwa muungano huo haujaarifu afisa wa polisi kuhusu mkutano huo.
''Hatujui kwamba kuna mkutano kama huo.hatujaarifiwa.
Kwa hivyo mtu yeyeto ambaye anadhani anaweza kufanya mkutano mkutano huo bila kuarifu polisi, mwambieni mtu huyo kwamba sheria itakabiliana na hali hiyo, alisema Koome''.

No comments:

Post a Comment