Thursday, November 9

UN yaonya hali mbaya ya binadamu Yemen

Bandari ya HodeidaImage, ambayo UN inaitumia sana kutawanya misaada YemenHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBandari ya Hodeida, ambayo UN inaitumia sana kutawanya misaada Yemen
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeuambia Muungano wa Jeshi linaloongozwa na Saudi Arabia nchini Yemen ni lazima kuruhusu misaada ya kibinadamu kupelekwa tena nchini humo.
Muungano huo wa jeshi umefunga njia zote za ardhini, anga na za maji tangu siku ya Jumatatu,kufuatia mashambulio ya makombora yaliyorushwa katika mji wa Riyadh na waasi wa Houthi walioko Yemen.
Baada ya mkutano wake wa ndani Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeagiza kuondolewa kwa vizuizi hivyo kwa kusema kwamba hali ya kibinadamu ni ya kutisha.
Mkuu wa shirika la misaada la Umoja wa Mataifa Mark Lowcock ameonya kutokea kwa kubwa la njaa, iwapo misaada haitapelekwa Yemen.
Hata hivyo Muungano huo wa Jeshi umedai kuwa vizuizi vinahitajika kuweza kuizuia Iran kuwapatia silaha waasi wa Ki-Houthi.

No comments:

Post a Comment